emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​Waziri Ridhiwani Kikwete Atembelea Banda la NSSF Katika Maonesho ya 49 ya Sabasaba



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ametembelea banda la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Sabasaba.

Katika ziara hiyo, Mhe. Kikwete aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Patrobas Katambi, pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Zuhura Yunus. Viongozi hao walipata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda hilo, ikiwa ni pamoja na elimu ya hifadhi skimu, elimu ya mafao, usajili wa wanachama wapya na huduma za kidigitali.

Aidha, ujumbe huo pia ulitembelea mabanda ya Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi na kiwanda cha Sisalana, ambavyo vinamilikiwa na NSSF.