emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​KUELEKEA SIKU YA UKIMWI DUNIANI DISEMBA MOSI 2024




Na MWANDISHI WETU,
Ruvuma. Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Bw. Yahya Mudhihir amewaongoza Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutoa elimu ya hifadhi jamii kwa wanachama na wananchi waliotembelea banda la Mfuko kwenye Maonesho ya kuelekea Siku ya UKIMWI duniani yanayoendelea katika Uwanja wa Michezo wa Majimaji Songea mkoani Ruvuma.
Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani mwaka 2024 yamebebwa na kauli mbiu isemayo “Chagua Njia Tokomeza Ukimwi”.

NSSF pamoja na kutekeleza majukumu yake ya msingi ikiwemo kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao pia inatekeleza Mwongozo wa kudhibiti VVU/UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza mahala pa kazi.

uchaguzi