emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

WAJUMBE WA BARAZA KUU LA WAFANYAKAZI NSSF WAPATIWA MAFUNZO


Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la 57 la Wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Bw. Masha Mshomba wamepatiwa mafunzo mbalimbali.

Mafunzo hayo yameendeshwa na watalaam mbalimbali na yalikuwa yanahusu masuala ya fedha na watoa huduma za fedha kama vile benki pamoja na wataalam wa saikolojia.

Lengo la kuendesha mafunzo hayo ni kuongeza uelewa kuhusu watoa huduma na huduma zinazotolewa kwa NSSF pamoja na wafanyakazi.

Mafunzo hayo yamefanyika leo tarehe 29 Oktoba 2026, katika ukumbi wa mikutano Cate Hotel mkoani Morogoro.