emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF YAENDELEA KUTOA HUDUMA NANENANE 2026 – TABORA



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaendelea kutoa huduma kwa wananchi katika Maonesho ya Nanenane 2026 yanayofanyika mkoani Tabora, chini ya kaulimbiu: "Tambua Soko: Ongeza Tija Kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050."


Kupitia ushiriki wake, NSSF inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za hifadhi ya jamii, ikiwemo elimu kuhusu mafao yanayotolewa na Mfuko, kuandikisha wanachama wapya, hususan kutoka sekta rasmi na wananchi waliojiajiri, kutoa elimu kuhusu njia rahisi za kujiunga kupitia simu ya mkononi popote walipo, kuelimisha kuhusu fursa za uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja, huduma za kidijitali ikiwemo NSSF Portal, pamoja na kutoa elimu ya kupambana na vitendo vya rushwa.