RAIS DKT. MWINYI AJIONEA BIDHAA ZA MIRADI YA KIMKAKATI YA NSSF SABASABA
- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, amejionea bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kupitia miradi ya kimkakati ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete alimkabidhi rasmi Rais Dkt. Mwinyi baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni tanzu za NSSF, ikiwa ni sehemu ya kuonesha mafanikio ya uwekezaji wa Mfuko katika sekta ya viwanda na uzalishaji wa bidhaa za ndani.