News
VIONGOZI MBALIMBALI NA WANANCHI WATEMBELEA NSSF KATIKA MAONESHO YA NANENANE DODOMA 2025

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao upo katika Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake unaendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na huduma mbalimbali katika Maonesho ya Nanenane 2025 yanayoendelea kitaifa Mkoani Dodoma ambapo viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wamepata nafasi ya kutembelea na kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo.
NSSF inashiriki maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kujisajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiajiri, elimu kuhusu kujichangia kupitia simu ya kiganganjani popote walipo, pia kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja, elimu kuhusu huduma za Mifumo mbalimbali ikiwemo Lango la Huduma (NSSF Portal) pamoja na elimu ya mapambano dhidi ya Rushwa