News
WAZIRI WA MADINI MHE. DOTTO BITEKO ATEMBELEA BANDA LA NSSF

Waziri wa Madini,Mhe. Dotto Biteko leo tarehe 1 Oktoba ,2022 ametembelea banda la NSSF katika Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya uwekezaji (EPZA)Bombambili Mkoani Geita.
Ambapo aliupongeza Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unavyohakikisha unatekeleza mpango wake wa kuyafikia makundi mbalimbali wakiwemo wachimbaji wadogowadogo wa madini katika maeneo mbalimbali.