News
NSSF Yatoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii Katika Mkutano wa Wahandisi

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshiriki katika Maonesho wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wahandisi katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Kupitia ushiriki huo, NSSF imeendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na kuhamasisha wanachama kutumia mifumo ya kidijitali ya Mfuko, ikiwemo NSSF Portal na NSSF App, ili kupata huduma mbalimbali kama vile taarifa za michango, kutengeneza kumbukumbu za namba za malipo (Control number), kulipia michango na kufungua madai.
Aidha, waajiri na wananchi waliojiajiri wamehimizwa kuhakikisha wanawasilisha michango yao kwa wakati, kwa lengo la kuongeza ufanisi wa hifadhi ya jamii na kuhakikisha mafao yanapatikana bila usumbufu.