News
NSSF Yaendelea Kufikia Makundi Mbalimbali katika Maonesho ya Biashara Kagera 2026
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaendelea kufikia makundi mbalimbali ya wajasiriamali na wananchi kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Biashara Kagera 2026, maarufu kama Maonesho ya Saba Saba, yanayoendelea katika Viwanja vya CCM, mkoani Kagera.
Kupitia maonesho hayo, wananchi na wadau wa biashara wanapata fursa ya kujifunza kuhusu umuhimu wa kujiunga na hifadhi ya jamii, namna ya kuchangia, pamoja na huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na wananchi waliojiajiri.
Banda la NSSF limeendelea kuvutia idadi kubwa ya wananchi wanaotembelea kupata elimu, ushauri na huduma mbalimbali, ikiwemo kujiandikisha na kuwa wanachama wa Mfuko.
NSSF imeeleza kuwa itaendelea kutumia majukwaa makubwa ya biashara na maonesho kama haya kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi wengi zaidi, kwa lengo la kuongeza uelewa na ushiriki wa Watanzania katika kujihakikishia maisha ya baadaye yenye usalama wa kipato.
MWISHO

