News
MICHEZO NSSF RUNNERS WASHIRIKI NBC DODOMA MARATHON
Timu ya riadha ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), tarehe 23 Julai, 2023, ilishiriki NBC Dodoma Marathon, yenye lengo la kuboresha Afya ya Mama na Mtoto, ambapo Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (MB) alikuwa mgeni rasmi na kuwapongeza wakimbiaji wa mbio hizo kwa kuchangia uboreshaji wa huduma ya afya ya mama na mtoto.
Mbio hizo zimehusisha wakimbiaji wa kilomita 5,10, 21 na 42. NSSF pamoja na kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao mbalimbali. Pia inashiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo ili kuimarisha afya za wafanyakazi na ushirikiano mahala pa kazi.

