NSSF Schemes
INFORMAL SECTOR
Mpango wa kitaifa wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) hutoa huduma za hifadhi ya jamii kwa wanachama walioajiriwa kwenye sekta binafsi na waliojiajiri wenyewe kwenye sekta isiyo rasmi chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018. Shirika limeanzisha mpango wa kitaifa wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi (National Informal Sector Scheme – NISS) kwa ajili ya kuwahudumia wanachama waliojiajiri wenyewe kwa urahisi, ufanisi na weledi.
Madhumuni ya kuanzisha mpango wa kitaifa wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi
- Kuongeza wigo wa wananchi kwa kutoa fursa ya hifadhi ya jamii kwa makundi ambayo hayanufaiki na huduma hizi ingawa wanashiriki kikamilifu kuchangia uchumi wa Nchi
- Kusaidia juhudi za Serikali za kupunguza umaskini wa kipato kwa wananchi
- Kuongeza nguvu za uzalishaji mali na kukuza uchumi wa Nchi
- Kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Wanufaika na mpango huu
- Mwananchi yeyote aliyejiajiri katika sekta isiyo rasmi kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wa madini, wafanyabiashara ndogondogo n.k.
- Walioko kwenye ajira na ambao wanapendelea kujiwekea akiba ya ziada chini ya mpango huu
- Waajiri wenye utaratibu wa mpango wa ziada kwa wafanyakazi wao (Employer based supplementary scheme)
- Waliolipwa mafao ya kukosa ajira na baada ya miezi 18 tangu walipwe mafao hayo hawakubahatika kupata ajira nyingine.
Namna ya kujiandikisha kuwa mwanachama
Kujiandikisha katika mpango wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi, mwanachama anatakiwa kuwa na vielelezo vifuatavyo;
- Awe na namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA) iwapo hana kitambulisho cha Taifa atatumia kitambulisho cha mpiga kura au leseni ya udereva
- Awe na picha moja
- Baadhi ya wanachama watatakiwa kutoa mchango wa awali usiopungua shilingi ishirini elfu (20,000/=) kama mchango wa mwezi.
Taratibu za kujiandikisha
- Mwanachama atatakiwa kujaza fomu ambayo imeambatanishwa na picha moja (passport size) kama hana namba au kitambulisho cha Taifa
- Baadhi ya wanachama watatakiwa kuwasilisha risiti ya malipo ya mchango wa awali.
Michango
- Mwanachama atachangia kiwango kisichopungua shilingi elfu ishirini (20,000/=) kwa mwezi au zaidi
- Kila mwanachama atatumia namba ya kumbukumbu ya malipo (Control Number) kuwasilisha michango.
Namna ya kuchangia
- Kupitia akaunti ya Benki au wakala
- Kupitia simu ya mkononi (mitandao yote)
Mafao
- Mafao yanayopatikana katika mpango wa kitaifa wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi ni;
- Mafao ya uzeeni (Old Age Pension)
- Mafao ya matibabu chini ya utaratibu maalumu
Huduma za mikopo
NSSF ina aina mbili ya mikopo kwa sekta isiyo rasmi:
1.Mikopo itolewayo kwa kushirikiana na Benki ya Azania pamoja na taasisi zingine za Umma kama vile NEEC, SIDO na VETA. Mikopo hii ni pamoja na;- Mikopo ya kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo na vya kati
Mikopo inayotolewa sasa ni ya uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda ambapo mtu mmoja mmoja au kikundi wanaweza kukopeshwa kuanzia shilingi milioni nane (8,000,000.00) hadi shilingi milioni mia tano (500,000,000.00).
- Mikopo ya Mitaji na
- Mikopo ya maendeleo na elimu
- Mikopo ya vitendea kazi
- Mikopo hii hutolewa kulingana na shughuli, biashara au sekta anayofanya kazi mwanachama husika. Mikopo hii itahusisha vitendea kazi kama vile vifaa, mashine, n.k. Vitendea kazi vitatolewa kwa mwanachama kama mafao au kwa njia ya mkopo wa gharama nafuu. Mikopo hii itatolewa kwa wanachama hai ambao wanachangia kwenye mpango wa kitaifa wa hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi. Sifa za kupata mkopo hutegemea uchangiaji na tabia ya mwanachama kuhusu usimamiaji wa biashara.