emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

Benefits

Social Health Insurance

Mafao haya hutolewa kwa mwanachama na wategemezi wake ambao ni mume/mke na watoto wasiozidi wanne wenye umri usiozidi miaka 18 au 21 ikiwa wapo shule.

Sifa zinazotakiwa

  • Mwanachama awe amechangia angalau michango ya miezi mitatu mfululizo karibu na kupata huduma ya matibabu
  • Makato ya asilimia 6 ya pensheni kwa wastaafu watakaotaka kupata huduma za matibabu baada ya kustaafu.

Mipaka katika Mafao ya Matibabu

  • Kulazwa kwa siku 42 kwa mwaka kwa familia
  • Matibabu ya dharura nje ya kituo/hospitali alichojiandikisha mwanachama anayesafiri kikazi si zaidi ya mara nne kwa mwaka kwa mgonjwa wa nje na si Zaidi ya masaa 48 mara mbili kwa mwaka kwa wagonjwa wanaolazwa.

Kukoma kwa huduma za matibabu

Huduma za matibabu katika mpango huu zinaweza kusitishwa mara moja kutokana na mambo yafuatayo:

  • Kifo cha mwanachama
  • Kuachishwa au kuacha kazi au kukoma kwa mkataba wa kazi
  • Kustaafu kwa hiari kwa umri wa kuanzia miaka 55 mpaka 59 au kustaafu kwa lazima kwa umri wa miaka 60
  • Kutowasilishwa kwa michango kwa zaidi ya kipindi cha miezi mitatu mfululizo
  • Kufikia umri wa zaidi ya miaka 18 au 21 kwa watoto.