Utangulizi
Utangulizi
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeanzishwa chini ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii Sura ya 50 marejeo ya mwaka 2018 kwa lengo la kutoa huduma ya Hifadhi ya Jamii kwa wafanyakazi walio katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.
Majukumu ya Mfuko
- Kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na isiyo rasmi
- Kukusanya michango
- Kuwekeza
- Kulipa mafao
Uandikishaji wanachama
Wanaotakiwa kisheria kuandikishwa kuwa wanachama wa NSSF ni
- Wafanyakazi walioajiriwa katika sekta binafsi
- Raia wa kigeni wanaofanya kazi Tanzania Bara
- Watumishi wa taasisi za kimataifa zinazofanya kazi Tanzania Bara
- Watu waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi
Uchangiaji
Viwango vya uchangiaji vya asilimia ya pato la mwezi
- Mwajiri 10% na Mfanyakazi 10%
- Mwajiri 15% na Mfanyakazi 5%
- Mwajiri anaweza kuchangia zaidi kuliko mfanyakazi
Uwekezaji
Shughuli za uwekezaji za Mfuko zinafanywa kwa mujibu wa Sera ya uwekezaji ya Mfuko kwa miongozo/kanuni za Benki kuu na Wizara yenye dhamana ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii.
Mafao
Mfuko unatoa mafao ya aina saba ambayo yamegawanyika katika makundi makuu mawili.
Mafao ya muda mrefu
- Pensheni ya uzee
- Pensheni ya ulemavu na
- Pensheni ya urithi
Mafao ya muda mfupi
- Msaada wa mazishi
- Mafao ya uzazi
- Mafao ya kupoteza ajira
- Huduma ya matibabu
Pensheni ni Mafao ya muda mrefu yatolewayo na Mfuko. Ni malipo ya kila mwezi kwa wastaafu, walemavu na warithi ili kurejesha upotevu wa kipato uliosababishwa na uzee, ulemavu au kifo.