News
NSSF MSHINDI WA KWANZA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII NA BIMA
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umepata tuzo baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Mifuko ya Hifadhi na Bima, kwenye Maonesho ya Saba ya ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita. Pichani, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde akimkabidhi tuzo hiyo Bi. Lulu Mengele, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF. Katikati ni Mhe. Martine Shigela, Mkuu wa Mkoa wa Geita.