emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF NA PSSSF WARAHISISHA HUDUMA KWA WANACHAMA NA WANANCHI KWA UJUMLAMFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSSF) wanashiriki maonesho ya 44 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam katika banda namba 13 lililopewa jina banda la ushirikiano kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.


Ushirikiano huo wa kutoa huduma pamoja umewarahisishia wanachama na wananchi kwa ujumla wanaofika kwenye maonesho hayo kwa lengo la kupata huduma itolewayo na Mifuko hiyo kwani itakumbukwa ya kwamba Mifuko ya hifadhi ya jamii iliunganishwa Agosti mwaka 2018 na kubaki Mifuko miwili tu ya hifadhi ya jamii PSSSF ikihudumia watumishi wa umma na NSSF ikihudumia watumishi wa sekta binafsi.


PSSSF ni muunganiko wa mifuko minne ya GEPF, LAPF, PPF na PSPF hivyo kumekuwa na kuhamishwa kwa wanachama kutoka Mfuko mmoja kwenda mwingine kulingana na mabadiliko ya ajira ya mhusika.

Ikiwa mhusika amehama kutoka ajira ya sekta binafsi kwenda ya umma, basi atalazimika kwenda “meza” ya PSSSF na kama amehama kutoka ajiya ya utumishi wa umma kwenda sekta binafsi atalazimika kwenda “meza” ya NSSF, hayo ndiyo manufaa ya kutoa huduma kwenye banda moja.