News
NSSF TUNAENDELEA KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII
Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata elimu ya hifadhi ya jamii katika banda namba 13 la NSSF katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), SabaSaba. Katika maonesho hayo NSSF inatoa elimu ya hifadhi ya jamii, usajili wa wananchi walio katika sekta isiyo rasmi, mifumo ya TEHAMA, mapambano dhidi ya rushwa, miradi ya uwekezaji na huduma za NSSF kidijitali.

