emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF YAMPA TUZO RAIS MHE. DKT SAMIA SULUHU HASSAN




*Ni kutambua mchango wake katika kufungua nchi na kuchagiza mafanikio ya NSSF katika kutoa huduma bora

*Huduma na mafao yanayotolewa na NSSF sasa kufanyika ndani ya saa 24

*Mkuu wa Mkoa wa Dodoma asema hajapokea malalamiko yeyote ya NSSF

Na MWANDISHI WETU,
Dodoma. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umempa tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kufungua milango ya uwekezaji pamoja na kuimarisha uchumi jambo lililochagiza mafanikio ya NSSF.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba amekabidhi tuzo hiyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule kwa niaba ya Mhe.Rais wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kilichofanyika tarehe 11 Oktoba 2024 jiji la Kiserikali la Dodoma.

Bw. Mshomba amesema mafanikio ambayo NSSF imeyapata yanatokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kutokana na kuchochea ukuaji uchumi, uwekezaji na mazingira mazuri ya biashara. “Haya yote yamechochea ongezeko la wanachama hadi kufikia 1,350,000 ukilinganisha na wanachama 750,000 waliokuwepo miaka mitatu iliyopita,” anasema Bw. Mshomba.

Anataja mafanikio mengine ambayo NSSF imepata kuwa ni utoaji huduma kwa wateja ambao umeimarika na hivi sasa mwanachama anaweza kuomba mafao na kulipwa ndani ya saa 24 ya kazi kutoka siku 30 au 14 zinazotambulika kisheria.

Pia, Mfuko umeongeza uwezo wa ukusanyaji wa michango, mapato ya uwekezaji yameongezeka pamoja na matumizi ya mifumo ya TEHAMA ambayo imerahisisha utoaji wa huduma kwa wanachama.

Kwa upande wake, Mhe. Senyamule ameupongeza Mfuko kwa hatua kubwa ulizopiga katika kuwahudumia wanachama. “Hongereni NSSF nikiri kuwa sijapokea kero yeyote hapa Dodoma inayohusu NSSF na hii inaonesha na kudhihirisha kuwa mnaendana na kauli mbiu ya Mkoa wetu inayosema ‘Kero Yako Wajibu Wangu’ nawapongeza sana NSSF,” anasema Mhe. Senyamule.

uchaguzi