emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF YATOA SEMINA KWA WAAJIRI WA SEKTA BINAFSI TEMEKE


Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Jokate Mwegelo amefungua semina kwa waajiri wa sekta binafsi iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Temeke, Dar es Salaam yenye lengo la kuwakumbusha majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuwasilisha michango kwa wakati.

Katika semina hiyo mada mbalimbali zilitolewa ikiwa ni pamoja na shughuli za Mfuko, Maboresho ya kanuni ya kikokotoo na Maboresho ya Mfumo wa Usajili na Uwasilishaji wa Michango kwa upande wa waajiri(employer portal) na huduma za mifumo kwa wanachama

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Cosmas Sasi aliwashukuru waajiri wa sekta binafsi kwa kushiriki semina hiyo ambapo pia aliwataka kutimiza wajibu wao wa kuwasilisha michango na kuwasajili wanachama wapya kwa mujibu wa Sheria.

Feruzi Mtika ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Temeke aliwashukuru waajiri kwa namna wanavyoshirikiana na Mfuko jambo ambalo limechangia mafanikio ya NSSF ambapo katika mwaka wa fedha uliopita Mfuko katika Mkoa wa Temeke ulikusanya shilingi bilioni 217 na kuandikisha asilimia 60 ya wanachama.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Lulu Mengele, alisema Mfuko unaendelea kutekeleza majukumu yakåe ya msingi ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ambao wanafanya shughuli kwenye sekta binafsi na makundi mbalimbali ili kuongeza uelewa wa hifadhi ya jamii