emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​NSSF YATUMIA FURSA YA UZINDUZI WA MPANGO KAZI WA TAIFA WA HAKI NA USTAWI KWA WATU WENYE UALBINO KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII



Na MWANDISHI WETU,

Uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Haki na Ustawi kwa Watu wenye Ualbino (MTHUWWU) na Mkakati wa Taifa wa Teknolojia Saidizi umezinduliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu wenye Ulemavu katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, tarehe 3 Desemba, 2024 ambapo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetumia hafla hiyo kuendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ikiwemo makundi mbalimbali ya Watu wenye Ulemavu

Kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya watu Wenye Ulemavu kwa mwaka huu ni 'Kukuza uongozi wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya mustakabali jumuishi na endelevu'.

Akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mkuu, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bi. Lulu Mengele amesema NSSF inashiriki hafla hiyo muhimu ikiwa ni sehemu ya kuendelea kutekeleza majukumu ya msingi ya Mfuko ambayo ni kuandikisha wanachama kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao.

Aidha Bi. Mengele amesema Watu wenye Ualbino na makundi mbalimbali ya wenye ulemavu ni wadau muhimu wa NSSF ambao pia ni wanachama wa Mfuko ambao kwa kutambua umuhimu wao, NSSF imeendelea kuwahakikishia mafao bora ikiwemo mafao ya ulemavu

uchaguzi