emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

USHIRIKI WA NSSF KATIKA MAONESHO YA FAHARI YA GEITA


Afisa Uhasibu Mwandamizi kutoka NSSF Bw. Robin Mwakyoma akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Mhe. Cornel Magembe (katikati) ambaye ni Mkuu wa Wilaya Geita, mara baada ya kutembelea banda la NSSF wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Nne Fahari ya Geita yaliyofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala.

NSSF inatumia maonesho hayo kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wanachama walioajiriwa katika sekta binafsi na wananchi waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi,kutoa elimu juu ya mapambano dhidi ya rushwa, kueleza umuhimu wa matumizi ya mifumo ya TEHAMA kwa mwanachama na mwajiri ili kumrahisishia huduma bila kulazimika kufika katika ofisi za NSSF, kusikiliza na kutatua kero za wanachama na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji ikiwemo miradi ya nyumba za kisasa na viwanja