News
WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NSSF GEITA
NSSF imezindua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja 2024, kauli mbiu isemayo 'Huduma Popote Ulipo', ambapo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Martine Shigela alikuwa mgeni rasmi. Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita, Bi. Winniel Lusingu, amewaongoza wafanyakazi na wateja katika uzinduzi huo. Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Meneja wa Sekta isiyo rasmi, Bi. Rehema Chuma pamoja na Afisa Mkuu Elimu kwa Umma, Bi. Janet Ezekiel.