emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF TUNAENDELEA KUTOA HUDUMA



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unashiriki na kutoa elimu ya hifadhi ya jamii katika Maonesho ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayoendelea viwanja vya General Tyre, Njiro Jijini Arusha.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Arusha, Josephat Komba, ametembelea maonesho hayo kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa, ambapo pia alitumia fursa hiyo kuhudumia wanachama waliofika katika banda la NSSF kwa ajili ya kupata huduma.

Katika maonesho haya, NSSF inatoa elimu ya hifadhi ya jamii, kusajili wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo rasmi, elimu kuhusu huduma za NSSF kidijitali, elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Uwekezaji na elimu kuhusu mafao.