News
NSSF Yashiriki Kikamilifu NBC Dodoma Marathon 2025

Timu ya riadha ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeshiriki mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika leo, tarehe 28 Julai 2025, katika Viwanja vya Jamhuri, jijini Dodoma.
Ushiriki wa NSSF katika mashindano hayo ni sehemu ya juhudi za Mfuko katika kuhimiza afya na ustawi wa wafanyakazi wake kupitia michezo, hususan katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa.
Mbio hizo zilihusisha watumishi wa NSSF kutoka ofisi mbalimbali za mikoa pamoja na Makao Makuu.
Mbali na majukumu yake ya msingi ambayo ni kuandikisha wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiajiri, kukusanya michango, kuwekeza na kulipa mafao, NSSF pia inaendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuwa karibu na jamii.
Mashindano haya ni miongoni mwa njia bora za kuhamasisha afya na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wafanyakazi wa umma na sekta binafsi nchini.
MWISHO