News
NSSF Yatoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii Mbeya Expo 2026
Mbeya
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Mbeya Expo 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya Uhindini mkoani Mbeya.
Kupitia maonesho hayo, yaliyoanza Mei 22 hadi 30, mwaka huu, wananchi mbalimbali wamepata fursa ya kujifunza kuhusu umuhimu wa kujiunga na Mfuko, namna ya kuchangia pamoja na huduma nyengine zinazotolewa na NSSF kwa wanachama wa sekta binafsi na wananchi waliojiajiri.
Banda la NSSF pia limetembelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali waliokwenda kujionea huduma na elimu inayotolewa kwa wananchi. Miongoni mwa viongozi hao ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Maryprisca Mahundi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa.
Aidha, Wakuu wa Wilaya ya Rungwe na Mbarali, Mhe. Jaffar Haniu na Mhe. Brigedia Jenerali Maulid Surumbu, walitembelea banda hilo na kupongeza jitihada za NSSF katika kuwafikia wananchi kupitia utoaji wa elimu ya hifadhi ya jamii.
Mbali na elimu, NSSF inaendelea kutoa huduma mbalimbali katika maonesho hayo ikiwemo uandikishaji wa wanachama wapya, uhakiki wa taarifa na michango pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali ya Mfuko.
NSSF imeeleza kuwa itaendelea kutumia majukwaa mbalimbali ya kitaifa kufikisha elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi ili kuongeza uelewa na ushiriki wa Watanzania katika huduma za hifadhi ya jamii.

