emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​RAIS DKT. SAMIA AIKABIDHI NSSF CHETI CHA SHUKRANI KWA MCHANGO WAKE KATIKA TAMASHA LA KIZIMKAZI 2026



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 14 Agosti 2026, amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba, Cheti cha Shukrani kwa kutambua ushiriki na mchango wa NSSF katika Tamasha la Kizimkazi 2026.

Cheti hicho ni ishara ya kutambua mchango wa NSSF katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza maendeleo ya taifa, kuimarisha ustawi wa wananchi na kuendeleza sekta ya hifadhi ya jamii.

Aidha, ushiriki wa NSSF katika tamasha hilo unaakisi dhamira ya Mfuko ya kuendeleza ujumuishaji wa wananchi katika fursa za kiuchumi na kijamii, sambamba na utekelezaji wa vipaumbele vya kitaifa vinavyoainishwa katika Dira 2050.