emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

Wastaafu wa Kagera Sugar Wahimizwa Kuendeleza Nidhamu ya Fedha Kabla ya Kustaafu


*Ni katika Semina ya maandalizi kabla ya Kustaafu Na Mwandishi Wetu, Kagera. Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeandaa semina maalumu kwa wastaafu watarajiwa wa kiwanda cha sukari cha Kagera, huku ukiwataka kuendeleza nidhamu ya fedha wakiwa bado kazini. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi, Kanali Mstaafu Khamis Maiga, wakati akifungua semina hiyo Januari 28, 2026. Kanali Mstaafu Maiga aliwataka wastaafu kuendeleza nidhamu ya kifedha wanayoitumia wakiwa kazini, ikiwemo kukatwa michango ya hifadhi ya jamii, kwani hili ndilo litakalowawezesha kuepuka matatizo ya kifedha baada ya kustaafu. Semina hiyo ililenga pia kuwapa elimu wastaafu watarajiwa kuhusu njia bora za kujiandaa kustaafu, mfumo wa ulipaji mafao na pensheni ya uzee pamoja na mambo ya msingi wanayopaswa kuzingatia na kuyaepuka kabla na baada ya kustaafu. Baadhi ya wastaafu watarajiwa wameshukuru NSSF kwa elimu hiyo, wakisema itawasaidia kupanga maisha yao vyema na kuepuka ushawishi wa watu wenye nia mbaya. Semina za namna hii ni mojawapo ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mfuko katika kuwaandaa wanachama wao kabla ya kustaafu.