News
WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NSSF KIDATU

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umezindua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2025 Kidatu, ikiwa na kaulimbiu isemayo “Kidijitali Tumeweza.”
Uzinduzi huo umeongozwa na Ramadan Kulunge Afisa msimamizi wa wilaya (DIO), ambaye aliwaongoza Wafanyakazi wa Mfuko na Wateja katika maadhimisho hayo yaliyolenga kuhamasisha utoaji wa huduma bora kwa njia za kidijitali na kuongeza huduma karibu na wanachama.