News
WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NSSF MASASI

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umezindua rasmi Wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka 2025 Masasi, ikiwa na kaulimbiu isemayo “Kidijitali Tumeweza.”
Uzinduzi huo umeongozwa na Bi. Hanna Mwangakala Afisa msimamizi wa wilaya (DIO), ambaye aliwaongoza Wafanyakazi wa Mfuko na Wateja katika maadhimisho hayo yaliyolenga kuhamasisha utoaji wa huduma bora kwa njia za kidijitali na kuongeza huduma karibu na wanachama.