emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

NSSF yatoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii katika Wiki ya Usalama Mahala pa kazi 2026 (OSHA) Mkoani Njombe


NSSF yatoa Elimu ya Hifadhi ya Jamii katika Wiki ya Usalama Mahala pa kazi 2026 (OSHA) Mkoani Njombe *Mpango wa Hifadhi Skimu wa NSSF wavutia wananchi waliojiajiri *Madereva Bodaboda na bajaji Mkoani Njombe wahamasika kujiunga na mpango huo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeshiriki katika katika Maonesho ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yaliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mjimwema, Mkoani Njombe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, akizungumza na maafisa usafirishaji wa bodaboda na bajaji waliopokea elimu ya hifadhi ya jamii na kujiunga na NSSF kupitia Skimu ya Hifadhi, ameeleza kuwa ni maono ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anawaachia tabasamu kundi hilo muhimu la waliojiajiri ambapo kupitia Hifadhi scheme, kundi hilo litaweza kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF kupitia michango yao wanayojiwekea kila mwezi. Aidha ameeleza kuwa Mhe. Dkt. Samia anataka maafisa usafirishaji hao wawe sehemu ya wanufaika katika Nguzo ya pili ya Dira ya Taifa ambayo inahusisha “Maisha bora na Ustawi wa watu wote” Mhe. Sangu ametoa rai kwa maafisa usafirishaji hao kuwa sehemu ya mabalozi wa kufikisha elimu hiyo walioipata kutoka NSSF kwa wenzao ili kuendelea kujichangia ili nao waweze kunufaika na mafao yanayotolewa na NSSF. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameipongeza NSSF kwa kufikia kundi hilo muhimu katika jamii ambapo ameeleza kuwa kupitia kujiunga NSSF, maafisa usafirishaji hao wanajijengea uwezo wa kuwa na uhakika ya kesho na NSSF inawajengea misingi ya kuiona kazi ya usafirishaji kuwa ni kazi kama kazi nyingine kwani kupitia kujiunga na Hifadhi Scheme itawapa kunufaika na mafao ya NSSF kama mtu alieajiriwa. Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele ameeleza kuwa kupitia ushiriki huo, NSSF imeendelea kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi na makundi mbalimbali, kuandikisha wanachama wapya pamoja na kuhamasisha wanachama waliopo kutumia mifumo ya kidijitali kupata huduma, ikiwemo mfumo wa NSSF Portal, NSSF App na USSD ( *152*00#) ambapo kupitia *152*00# mwanachama anaweza kujiunga na kuwasilisha michango yake ya kila mwezi popote alipo bila kulazimika kufika Ofisi za NSSF.