emblem

The United Republic of Tanzania

National Social Security Fund (NSSF)

We Build Your Future

News

​WANACHAMA WAFURIKA BANDA LA NSSF SABASABA KUPATA HUDUMA BORA; WENYEWE WAPONGEZA ELIMU WANAYOPATA, WANANCHI WAENDELEA KUJIUNGA



Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) unaendelea kutoa huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) katika banda namba 13. Katika maonesho hayo, wananchi mbalimbali wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na Mfuko ikiwemo elimu ya hifadhi ya jamii, usajili wa wananchi waliojiajiri, elimu ya mafao, mifumo ya TEHAMA, mapambano dhidi ya rushwa, miradi ya uwekezaji na huduma za NSSF kidijitali.